Hofu Yazidi Kwa Familia Ya Kijana Aliyeuliwa Kinyama Mtaani Likoni.

Hofu Yazidi Kwa Familia Ya Kijana Aliyeuliwa Kinyama Mtaani Likoni.

by -
0 742

Mwanamke aliyejeruhiwa akijaribu kumnusuru kakake mdogo aliyeuawa mtaa wa Likoni hapa Mombasa kwa kuchinjwa na mtu asiyejulikana ,sasa anasema anahofu kurudi nyumbani licha ya kuondoka hospitalini.

Kaha Hassan mwenye umri wa miaka 30, alisema anaogopa kurudi kwao Likoni, kwa kuwa muuwaji wa kakake bado hajatambuliwa.

Mwanamke huyo alilazwa hospitalini mapema wiki hii baada ya kukatwa mkono akijaribu kumwokoa nduguye ambaye alichinjwa hadi kufariki.

Mvulana huyo wa miaka 14 kwa jina Hassan Bakari, aliuawa kwa kukatwa upanga na mtu ambaye hajatambuliwa hadi sasa akiwa amelala nyumbani kwao usiku wa jumapili mtaa wa Ebenezer Likoni hapa Mombasa.

Comments

comments