Wazee Waliotuhumiwa Kwa Uchawi Huko Kilifi Sasa Wahofia Njaa.

Wazee Waliotuhumiwa Kwa Uchawi Huko Kilifi Sasa Wahofia Njaa.

by -
0 1121

Wazee wanaotuhumiwa kuwa wachawi ambao wanahifadhiwa katika kaya Godoma huko Mrima wa Ndege, Ganze kaunti ya Kilifi,wanahofia kupoteza maisha kutokana na makali ya njaa.

Wazee hao wanasema tangu kifo cha mfadhili wao Mangi Mitsanze wiki mmoja iliopita, wamelazimika kulala njaa mara kadhaa baada ya familia ya marehemu kusitisha kutoa chakula.

Wakiongozwa na mzee Thomas Kenga, wazee hao walieleza kuwa kwa sasa wanalazimika kuombaomba chakula kwa wasamaria wema huku mara nyingine wakilazimika kujitafutia licha ya umri wao mkubwa.

Kenga aliongeza kwamba endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuwakwamua wazee hao katika janga hilo la njaa, basi huenda wakapoteza maisha.

Marehemu Mangi Mitsanze, atazikwa mnamo umamosi tarehe 9 nyumbani kwake Mrima wa Ndege, baada ya mwili wake kutembezwa katika uwanja wa Karisa Maitha na Kaya Godhoma kupewa heshima ya mwisho kutoka kwa wananchi.

Comments

comments