Wawili wafariki katika ajali Voi.

Wawili wafariki katika ajali Voi.

by -
0 1224

Watu wawili wamefariki na wengine sita kujeruhiwa katika ajali ya barabarani eneo la Man Eaters huko Voi, usiku wa kuamkia leo.

Ajali hiyo imetokea baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na trela kwenye barabara kuu ya Mombasa kulekea Nairobi.

Kamanda wa polisi wa trafiki eneo hilo Richard Bitonga, amesema huenda dereva wa basi alikuwa anasinzia ama alikuwa anajaribu kupita trela hilo.

Bitonga amesema dereva wa basi ambaye alinusurika katika ajali hiyo, alitoroka na alikuwa anasakwa.

Majeruhi wanapokea matibabu katika hospitali kuu ya Voi.

Comments

comments