Viongozi Wa Jumuiya Ya Kaunti Za Pwani Waanza Mkutano Mombasa.

Viongozi Wa Jumuiya Ya Kaunti Za Pwani Waanza Mkutano Mombasa.

by -
0 525

Viongozi wa jumuiya ya kaunti za pwani wameanza mkutano hapa Mombasa kukutana na wadau wa sekta ya kibinafsi.

Jumuiya hiyo ambayo inahusisha magavana wa eneo la pwani inanuia kushirikisha sekta ya kibinafsi kwa lengo la kuinua uchumi wa eneo hili.

Wadau hao wa sekta ya kibinafsi wanatoa maoni na mapendekezo yao kujaribu kubuni mbinu zaidi za kuleta maendeleo kwa ushirikiano na serikali za kaunti za pwani.

Mwenyekiti Salim Mvurya alisema wametambua jinsi sekta ya kibinafsi ni muhimu katika juhudi za kuinua uchumi wa pwani.

Miongoni mwa magavana waliohudhuria mkutano huo ni gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jefwa Kingi na gavana wa Lamu Issa Timamy.

Comments

comments