Wawili Wakana Shtaka la Mauaji Majengo.

Wawili Wakana Shtaka la Mauaji Majengo.

by -
0 308

Mahakama kuu mjini Mombasa inajiandaa kusikiza kesi ya mauaji inayowakabili watu wawili wanaume, wanaodaiwa kumuua mtu mmoja eneo la Majengo, miaka mitatu iliyopita.

Jaji Martin Muya alisema ataanza kusikiza kesi hiyo mnamo May 21, kuhusiana na mauaji ya Mohammed Usi, Februari mwaka wa 2012.

Washtakiwa hao Rashid Bakari Juma na Yusuf Abdukadir walikana mashtaka hayo, mbele ya jaji wa Mombasa Martin Muya.

Mshtakiwa wa kwanza Rashid Juma alipewa dhamana ya shillingi laki tano, kutoka rumande waakti kesi ikiendelea kusikizwa.

Mahakama itaamua Machi tarehe 18 iwapo mshtakiwa wa pili atapewa dhamana, au atasalia rumande waakti kesi hiyo ikiendelea kusikizwa.

Comments

comments