Shule Ya Upili Ya Voi Girls Yataka Fidia Zaidi.

Shule Ya Upili Ya Voi Girls Yataka Fidia Zaidi.

by -
0 440

Shule ya upili ya wasichana ya Voi,kaunti ya Taita Taveta iliyoathirika na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa, sasa inadai kuwa fidia iliyotengewa ni kidogo.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mary Mwasaru, alisema shilingi milioni 5 wanayotarajiwa kupewa haitatosha kwa ujenzi wa shule mpya.

Mwasaru alisema kiwango hicho kitatosha kufidia ekari 1 tu ya ardhi na kwamba sasa wameiandikia barua tume ya kitaifa ya ardhi nchini kutathmini suala hilo.

Takriban shule 11 kaunti ya Kwale na Taita Taveta zitabomolewa ili kupisha mradi huo wa ujenzi wa reli ya kisasa.

Baadhi ya shule hizo ni kama Julani na Mavumbo, Voi girls na shule ya msingi ya Msharinyi.

Comments

comments