Mwanamume Akamatwa Kwa Kujifanya Mwanamke.

Mwanamume Akamatwa Kwa Kujifanya Mwanamke.

by -
0 436

Polisi mtaa wa Likoni-Mombasa inasema imemkamata mwanaume ambae amekuwa akishukiwa kujifanya mwanamke na kufanya kazi ya nyumba katika mtaa wa Majengo Mapya.

Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye anajiita Mary Ann aliajiriwa kama kijakazi katika familia moja mtaani humo bila ya familia hiyo kufahamu alikuwa mwanaume.

Hata hivyo ujanja wake uling’amuliwa na mvulana mdogo aliyekuwa akilala na mshukiwa ambaye aliwafahamisha wazazi wake na kupiga ripoti kwa polisi.

Mkuu wa polisi wilayani Likoni Willy Simba alisema maafisa wa C.I.D wangali wanamhoji mshukiwa kabla ya kufunguliwa mashtaka.

Comments

comments