Mahakama Yaagiza Mshukiwa Feisal Mohammed Apelekwe Hospitalini

Mahakama Yaagiza Mshukiwa Feisal Mohammed Apelekwe Hospitalini

by -
0 297

Mahakama moja hapa Mombasa imeagiza idara ya magereza kumpeleka hospitali mara moja mshukiwa wa ulanguzi wa pembe za ndovu, aliyelalamikia kuugua kwa miezi kadhaa.

Hakimu Justus Kituku aliagiza afisa mkuu wa gereza la Shimo La Tewa kuwasilisha ripoti ya matibabu ijumaa wiki ijayo, kabla ya mahakama kuamua iwapo Feisal Mohammed atapewa dhamana au la.

Wakili wake Gerald Magolo na wakili wa serikali walijibizana mahakamani baada ya ripoti kuonesha kuwa Feisal alitibiwa kama ilivyoagizwa na mahakama awali, lakini Feisal alisema daktari wake binafsi alikataliwa.

Alikamatwa nchini Tanzania mwezi Disemba mwaka jana kupitia polisi wa InterPol, akidaiwa kuwa mshukiwa mkuu katika kesi ya ulanguzi wa pembe inayokabili washukiwa 9.

Comments

comments