Boinett Ajipigia Debe.

Boinett Ajipigia Debe.

by -
0 318

Utepetevu miongoni mwa maafisa wa usalama umetajwa tena, kuwa maafisa wa polisi walikosa kuokoa maisha huko Mpeketoni kaunti ya Lamu, wakati wa mashambulio ya kigaidi ambapo watu wengi waliuawa mwaka jana.

Katika mkutano wa bunge la kitaifa na lile la Senate, wabunge walikariri kuwa polisi walipashwa habari kuhusu njama ya mauaji huko Mpeketoni lakini wakapuuza.

Walikuwa wakizungumza Alhamisi asubuhi mjini Nairobi katika kikao cha kumhoji Joseph Boinett – ambaye aliteuliwa kuchukua wadhifa wa Inspekta mkuu wa Polisi.

Boinett aliambia jopo hilo iwapo atafanikiwa kuwa Inspekta mkuu wa polisi, atasaidia kuziba mwanya uliopo baina ya Polisi na idara ya ujasusi.

Nafasi ya Inspekta mkuu wa polisi nchini Kenya ilisalia wazi mwishoni mwa mwaka jana 2014, baada ya David Kimaiyo kujiuzulu kutoka wadhifa huo.

Comments

comments