Bastola Ya Polisi Yatumika Kwa Wizi

Bastola Ya Polisi Yatumika Kwa Wizi

by -
0 303

Idara ya polisi hapa Mombasa imesema bastola iliyopatikana alhamisi hii kutoka kwa washukiwa wawili wa wizi waliouawa baada ya kupigwa risasi hapa Mombasa, iliibwa kutoka afisa mmoja wa polisi mjini Nairobi.

Bastola hiyo aina ya Ceska ambayo ilikuwa imesajiliwa, iliibwa kutoka kwa afisa huyo wa cheo cha koplo akiwa katika mkahawa.

Taarifa za polisi zilisema kuwa kundi hilo la majambazi limekuwa likutumia bastola hiyo kutekeleza uhalifu na kuhangaisha wakaazi hapa Mombasa.

Lakini kundi hilo sasa limedaiwa kusambaratika baada ya viongozi wao wakuu wawili kuuawa na polisi.

Mapema mwezi jana mtu aliyetajwa kama kiongozi wa kundi hilo, aliuawa na polisi katika mtaa wa Kizingo hapa Mombasa.

Comments

comments