Washukiwa wa Ujambazi wauawa Mombasa.

Washukiwa wa Ujambazi wauawa Mombasa.

by -
0 424

Washukiwa wawili wa ujambazi wameuawa Alhamisi mchana kwa kupigwa risasi na polisi huku mmoja akitoroka katika barabara ya Moi Mjini Mombasa.

Yasemekana Washukiwa hao watatu waliokuwa kwenye pikipiki walinuia kutekeleza wizi katika duka moja la kuuza magari.

Polisi wamempiga risasi mshukiwa aliyekuwa akiendesha pikipiki kabla ya pikipiki hiyo kupoteza mwelekeo na kuanguka.

Mshukiwa wa pili ameuawa karibu na duka la Toyota Kenya alipokuwa akijaribu kutoroka.

Mkuu wa upelelezi eneo la pwani Henry Ondiek amesema wamepata bastola moja, majarida mawili na leseni za gari zinazoshukiwa kuwa za wizi kutoka kwa washukiwa hao.

Comments

comments