Vijana Pwani Kushauriwa Kutojiunga Na Makundi Haramu.

Vijana Pwani Kushauriwa Kutojiunga Na Makundi Haramu.

by -
0 632

Viongozi kaunti ya Kilifi wameanzisha harakati za kutoa ushauri nasaha kwa vijana dhidi ya kujiunga na makundi ya kigaidi.

Mbunge wa Ganze -Peter Shehe ambaye pia ni msemaji wa jamii ya Kaya, alisema serikali ya kaunti ya Kilifi itatoa nafasi za ajira kwa vijana kama njia moja ya kuwaepusha na makundi hayo.

Viongozi hao walisema makundi hayo ni hatari kwa vijana, kwani huwadanganya kujiunga kwa kuwaahidi ajira.

Hapa pwani vijana kadhaa waliripotiwa kutorokea nchi jirani ya Somalia kujiunga na kundi la kigaidi la Al-shabaab.

Kulingana na shirika la kijamii kuhusu usalama na maendeleo KECOSCE, vijana hao hushawishiwa kwa pesa na anasa zingine kujiunga na Al-shabaab.

Comments

comments