Nairobi Yaongoza Katika Visa vya Uhalifu Nchini.

Nairobi Yaongoza Katika Visa vya Uhalifu Nchini.

by -
0 643

Takwimu za hivi punde zinaonesha kuwa jiji la Nairobi linaongoza katika visa vya uhalifu kote nchini.

Ripoti hiyo ya idara ya Polisi, inaonyesha kuwa Nairobi imeshuhudia takriban visa elfu saba vya uhalifu, katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Visa hivyo ni pamoja na mauaji, wizi wa magari, utekaji nyara, na watu kushikwa kabari na wakora mitaani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo Isiolo imeorodheshwa kama kaunti yenye visa vichache zaidi vya uhalifu, ikiwa na takriban visa 300 katika muda wa mwaka mmoja uliopita.

Mombasa, Mandera na Lamu zimeorodheshwa pia kuwa miongoni mwa maeneo yenye utovu wa usalama.

Comments

comments