Mshukiwa Alilia Mahakama Juu Ya Matibabu.

Mshukiwa Alilia Mahakama Juu Ya Matibabu.

by -
0 256

Mshukiwa wa ulanguzi wa pembe za ndovu aliyeomba mahakama imruhusu kutibiwa nje ya rumande iliyo katika gereza la Shimo La Tewa, ameambia mahakama hiyo kuwa bado hajatibiwa.

Mshukiwa kupitia wakili wake Jared Magolo aliiomba mahakama atibiwe nje ya rumande kufuatia hali yake mbaya ya kiafya.

Awali mahakama ilikataa ombi la mshukiwa ikisema atibiwe akiwa rumande gerezani Shimo La Tewa, kutokana na uzito wa kesi inayomkabili.

Mahakama ilitarajiwa kupokea ripoti kuhusu matibabu ya mshukiwa kabla ya kesi hiyo kuendelea.

Naye wakili wa serikali Alexander Muteti aliambia mahakama licha ya kuwa mshukiwa anaweza kupewa ulinzi wa maafisa wa polisi, ni bora daktari amtembelee na kumtibu akiwa rumande.

Feisal Mohammed alikamatwa nchini Tanzania na Polisi wa kimataifa -Interpol kwa madai ya kupatikana na tani tatu za pembe za ndovu, zilizokuwa zimefichwa katika bohari moja eneo la Tudor kaunti ya Mombasa, Juni mwaka 2014.

Comments

comments