Mijengo Kupitia Mfumo Wa Elektroniki Mombasa.

Mijengo Kupitia Mfumo Wa Elektroniki Mombasa.

by -
0 807

Serikali ya kaunti ya Mombasa inatarajiwa kuzindua mfumo wa ki-elektroniki, wa kutoa leseni za watu wanaojihususha na ujenzi.

Kupitia mfumo huo wataalamu wa ujenzi kama vile Masoroveya na wahandisi, watapata taratibu za kuanzisha majengo katika mitandao.

Mfumo huo kwa ushirikiano na Benki ya Dunia, unatarajiwa kupunguza muda unaotumiwa kupata leseni na pia kuongeza mapato kwa serikali ya kaunti.

Afisa mkuu katika wizara ya ardhi na nyumba katika kaunti ya Mombasa Jabu Salim, amesema kupitia mfumo huo hatari ya majumba kuporomoka itapungua.

Comments

comments