Matokeo Ya KCSE Kutolewa Wiki Ijayo.

Matokeo Ya KCSE Kutolewa Wiki Ijayo.

by -
0 797

Matokeo ya mtihani wa KCSE mwaka uliopita wa 2014, unatarajiwa kutangazwa Jumanne wiki ijayo, Machi tarehe 3.

Waziri wa Elimu Profesa Jacob Kaimenyi anatarajiwa kutangaza rasmi matokeo hayo ya mtihani wa kidato cha NNE uliofanyika kote nchini mwishoni mwa mwaka jana.

Zaidi ya watahiniwa laki nne humu nchini walifanya mtihani huo, unaotumiwa kila mwaka kuteua wanafunzi watakaojiunga na vyuo vikuu nchini.

Kando na watahiniwa raia wa Kenya, kuna wanafunzi waliofanya mtihani huo wakiwa kama wakimbizi, hasa kutoka nchi ya Sudan Kusini.

Comments

comments