Keriako Tobiko Awasilisha Taarifa Kuhusu Mauaji Ya Mpeketoni.

Keriako Tobiko Awasilisha Taarifa Kuhusu Mauaji Ya Mpeketoni.

by -
0 507

Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya Umma Keriako Tobiko amewasilisha mahakamani taarifa za mashahidi 34, kuhusiana na kesi ya mauaji yaliyokumba Mpeketoni-Lamu mwaka jana.

Stakabadhi hizo zimewasilishwa mahakamni Mombasa kupitia wakili wa serikali Alexander Muteti, baada ya kesi hiyo kukosa kuanza kusikizwa kutokana na ukosefu wa taarifa za mashahidi.

Awali mshukiwa mkuu katika kesi hiyo kupitia wakili wake, alitishia kushtaki serikali, kwa kuchelewesha ushahidi.

Wakili wake Taib Ali Taib ameambia mahakamani kuwa tayari wamepokea stakabadhi hizo, na hakimu Martin Muya akaagiza kesi isikizwe kuanzia Aprili tarehe 15.

Katika kesi hiyo Mahad Swaleh maarufu “Jesus” na dereva wa matatu Dyana Salim, wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 60 kuhusiana na mauaji ya watu wengi huko Mpeketoni kaunti ya Lamu.

Comments

comments