Jumuia ya Pwani Kukutana na Sekta ya Kibinafsi

Jumuia ya Pwani Kukutana na Sekta ya Kibinafsi

by -
0 304

Viongozi wa muungano wa Jumuiya ya Pwani wanatarajiwa kukutana na wadau wa sekta ya uwekezaji wa kibinafsi wikiendi hii kuzungumzia masuala ya uchumi wa pwani.

Mwenyekiti wa jumuia hiyo Salim Mvurya anasema mkutano huo utafanyika katika chuo kikuu cha–TUM hapa Mombasa, na pia utatoa fursa kwa makundi mengine yenye nia ya kujiunga na jumuiya ya pwani.

Mvurya amedokeza kuwa wahusika wa sekta ya kibinafsi wameonesha nia ya kujiunga na jumuia hiyo, na ni kiungo muhimu katika uchumi wa ukanda wa pwani.

Wengine wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo ni muungano wa watengenezaji bidhaa nchini, wamiliki wa hoteli, muungano wa wachukuzi pamoja na chama cha wanasheria nchini LSK.

Comments

comments