Polisi Mombasa Wasaka Majambazi

Polisi Mombasa Wasaka Majambazi

by -
0 1395

Maafisa wa polisi wameanzisha msako dhidi ya watu wanaoaminika kuwa majambazi waliovamia duka moja la kuuza dawa eneo la bombolulu kaunti Mombasa na kuiba pesa usiku wa kuamkia Ijumaa.

Watu hao wanne walijifanya wateja, lakini baadaye wakageuka na kumwamrisha mwenye duka kuwapa pesa zote.

Taarifa za polisi zinasema kuwa walimjeruhi kwa kumpiga risasi mpita njia aliyekuwa karibu na duka hilo kabla ya kutoroka kutumia pikipiki.

Hayo yanakuja huku washukiwa wengine wa ujambazi wakiripotiwa kuhangaisha wafanyabiashara mtaa wa magorofani, Mshomoroni.

Comments

comments