Mwili Wa “Yebei” Wapatikana Tsavo

Mwili Wa “Yebei” Wapatikana Tsavo

by -
0 351

Idara ya polisi imesema inachunguza endapo mwili uliopatikana katika mbuga ya Tsavo kaunti ya Taita Taveta ni wa mtu anayesemakana kuwa shahidi wa mahakama ya kimataifa ya jinai ICC-Meshack Yebei.

Wataalam kutoka kikosi cha polisi walisema watashirikiana na familia ya Yebei kuutambua mwili huo.

Yebei alitoweka nyumbani kwake mjini Eldoret kwa njia ya kutatanisha mwezi disemba mwaka jana, baada ya kutekwa nyara na watu wasiojulikana, akielekea dukani.

Mwezi januari mwaka huu mwili uliodhaniwa kuwa wa Yebei, ulipatikana katika mto Yala kilomita 40 kutoka nyumbani kwao,lakini siku chache baadae familia nyingine ilijitokeza na kuudai mwili huo.

Familia hiyo ilikabidhiwa mwili baada ya uchunguzi wa polisi kubaini kuwa mwili huo haukuwa wa Meshack Yebei.

Comments

comments