Wakazi Wa Lamu Waanza Kupokea Fidia

Wakazi Wa Lamu Waanza Kupokea Fidia

by -
0 639

Serikali kuu hatimaye imeanza kulipa fidia ya shilingi millioni 860 kwa waathiriwa wa mradi wa ujenzi wa Bandari mpya ya Lamu-Lapset.

Mukurugenzi mkuu mtendaji wa mradi huo Sylvester Kasuku alisema fedha hizo tayari zimetumwa katika akaunti za benki za waathiriwa hao na kiwango kilichosalia kitatolewa baada mambo kadhaa kukamilika.

Kasuku alisema pesa hizo zilitolewa mapema wiki hii na zilikuwa zikihifadhiwa na mamlaka ya bandari nchini KPA ili kusubiri mipango yote kukamilika.

Waathiriwa hao wamekuwa wakililia fidia kwa zaidi ya miaka miwili sasa na kupelekea wengi kuandamana mjini humo.

Comments

comments