Usajili Wa Wasio Na Uraia Waendelea Msambweni

Usajili Wa Wasio Na Uraia Waendelea Msambweni

by -
0 445

Zoezi bado linaendelea kusajili watu wasio na uraia huko kusini mwa pwani.

Zoezi hilo lilianza wiki jana huko Kinondo wilaya ya Msambweni na maafisa wa serikali wanaoendesha zoezi hilo wanatarajiwa kukamilisha usajili eneo hilo la Kinondo jumanne tarehe 17.

Wataelekea Ukunda na sehemu zingine kusini mwa pwani kuanzia jumatano tarehe 18.

Wanaosajiliwa kupata uraia wa Kenya ni wale wahamiaji ambao hawana vitambulisho wengi wakiwa wa-makonde waliohamia Kenya kutoka nchini Msumbiji.

Comments

comments