Wanafunzi Watiliwa Mihadarati Kwenye Chakula-NACADA

Wanafunzi Watiliwa Mihadarati Kwenye Chakula-NACADA

by -
0 1900

Halmashauri ya kupambana na dawa za kulevya nchini NACADA,imesema imeanza uchunguzi kuhusu visa ambapo baadhi ya vyakula vinavyouziwa watoto wa shule za msingi zinachanganywa na mihadarati.

Mkurugenzi mkuu wa halmashauri hiyo Dr. Willian Okedi alisema kuliibuka madai kuwa baadhi ya vyakula hivyo huchanganywa na dawa za kulevya.

Okedi alisema walanguzi wa dawa hizo wamekuwa wakitia dawa kwenye vyakula vinavyopendwa na watoto kama vile keki,peremende na hata viazi karai.

“Hawa watu wanajua vyakula ambavyo watoto wanapenda sana, ndio maana wameanza kuwatilia dawa za kulevya,hapa pwani wanatumia sana viazi”,Okedi alisema.

Mkurugenzi huyo wa NACADA alisema watatoa ripoti yao baada ya uchunguzi huo ili hatua mwafaka zichukuliwe mapema.

Eneo la pwani limekuwa likikumbwa na tatizo la uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya.
.

Comments

comments