Wakazi wa Lamu Wataka Ushauri Namna Ya Kutumia Pesa Za Fidia.

Wakazi wa Lamu Wataka Ushauri Namna Ya Kutumia Pesa Za Fidia.

by -
0 464

Baraza la wazee wa kaunti ya Lamu linaitaka serikali kuu ianzishe kampeni ya kuwaelimisha waathiriwa wa mradi wa ujenzi wa Bandari ya Lamu, namna ya kutumia mamilioni ya pesa watakazolipwa kama fidia.

Baraza hilo lilisema huenda watakaofidiwa wakatumia vibaya fedha hizo, badala ya kuzitumia kujiendeleza kimaisha.

Mwenyekiti wa baraza hilo la wazee, Shariff Kambaa alisema wakazi wengi wa Lamu wanaishi katika umaskini, na huenda wakajiingiza kwenye anasa punde baada ya kupokea pesa hizo za fidia.

Kila mwathiriwa aliyepeana ardhi yake kwa mradi huo wa ujenzi wa bandari, anatarajiwa kufidiwa kwa shilingi milioni 1.5 kwa kila ekari moja ya ardhi.

Comments

comments