Waathiriwa wa LAPSSET kulipwa Juma Lijalo.

Waathiriwa wa LAPSSET kulipwa Juma Lijalo.

by -
0 434

Serikali ya kaunti ya Lamu imesema wakaazi wa kaunti hiyo ambao ardhi yao ilitwaliwa kwa ajili ya ujensi wa bandari mpya ya Lamu, watapokea fidia yao juma lijalo.

Gavana Issa Timamy amesema mipangilio yote imekamilika na kwamba kilichosalia ni ramani za kila kipande cha ardhi zitakazowezesha utengenezaji wa hati miliki kabla ya malipo hayo kutekelezwa.

Timamy amesema yeye na maafisa wengine wa kaunti hiyo walikutana na mweneyekiti wa tume ya kitaifa ya ardhi Muhammad Swazuri Jumatano iliyopita na aliwahakikishia malipo yatafanywa karibuni.

Comments

comments