Maskwota Lamu Waandamana dhidi ya Unyanyasaji na Maafisa wa Misitu .

Maskwota Lamu Waandamana dhidi ya Unyanyasaji na Maafisa wa Misitu .

by -
0 328

Mamia ya maskwota kutoka ziwa Amu na Kiongwe huko Mpeketoni kaunti ya Lamu wameandamana wakidai kuhangaishwa na maafisa wa kulinda misitu KFS.

Maskwota hao zaidi ya 500, wanadai maafisa hao wamewafurusha kutoka ardhi ambayo wanasema wameimiliki kwa miaka mingi, mbali na askari hao kuwapiga na hata kuchoma nyumba zao.

Wamesema walifurushwa kutoka kwa ardhi hiyo hata baada ya naibu gavana wa kaunti hiyo Eric Mugo, kushauri idara ya misitu kusubiri shughuli ya usoroveya ikamilishwe katika ardhi hiyo kabla ya kuchukua hatua zozote.

“Wanatufurusha wakidai tumeingia kwa ardhi ya wenyewe,Lakini tumekua tukiishi hapa kwa miaka mingi sasa na hatutaondoka hadi wizara ya ardhi itutaftie ardhi nyingine ya kuishi,” msemaji wao amesema.

Asilimia 60 ya ardhi ya Lamu bado inatambulika kama ardhi ya umma, kauli ambayo maskwota wanadai imetoa mpenyo kwa wanyakuzi na mabwenyenye kunyakua ardhi hiyo.

Juhudi za kuwasiliana na idara ya misitu hazikufaulu.

Comments

comments