Waakazi Kilifi Waonywa dhidi ya Mauaji ya Washukiwa wa Uchawi.

Waakazi Kilifi Waonywa dhidi ya Mauaji ya Washukiwa wa Uchawi.

by -
0 398

Polisi katika kaunti ya Kilifi wameonya wakaazi eneo hilo dhidi ya kuwauwa kiholela watu wanaowashuku kuwa wachawi.

Afisa mkuu wa polisi wilayani Ganze, Alexander Makau amesema wakaazi wamekuwa wakitekeleza mauaji kwa visingizio vya uchawi na udanganyifu katika ndoa, mienendo aliyotaja kama ukiukaji wa sheria.

Haya yanajiri siku moja baada ya mwanamume kuvamiwa na kuuawa na umati eneo hilo kwa madai alikuwa na mazoea ya kutembea na wake za watu.

Visa vya washukiwa wa uchawi kuuawa Kilifi vimekuwa vikiripotiwa na vimehusisha kuchomwa kwa nyumba na mali ya washukiwa.

Wazee kadhaa eneo hilo wamelazimika kutorokea usalama wao, kwa kuhofia kuvamiwa.

Comments

comments