Shule Yafungwa Kilifi Kufuatia Mgomo.

Shule Yafungwa Kilifi Kufuatia Mgomo.

by -
0 361

Shule ya upili ya Msumarini iliyo Kikambala kaunti ya Kilifi imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kugoma.

Mkurugenzi wa elimu kaunti ya Kilifi Dickson Ole Keis amesema wanafunzi hao wamegoma wakitaka mwalimu mkuu aondolewe kwa kile wanachokitaja kama kushindwa kuiendeleza kimasomo.

Ameongeza kuwa wanafunzi hao wanataka basi la shule, maabara ya kisasa, uwanja wa soka na ukumbi mkubwa wa maankuli.

Polisi wanashika doria katika shule hiyo kutokana na jaribio la wanafunzi kutaka kuchoma ofisi ya mwalimu mkuu.

Katika kisa tofauti, shule ya upili ya wasichana ya Moi Kadzonzo wilayani Kaloleni Kaunti ya Kilifi ilichomeka jumatano usiku.

Kulingana na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Doris Kavuku, moto huo unaokisiwa kutokana na hitilafu za nguvu za umeme ulizuka saa kumi na moja alifariji na kuteketeza mali ya thamani kubwa katika bweni moja.

Kavuku amesema miongoni mwa mali iliyoteketea ni paa la bweni, kuta na magodoro.

Wakuu wa shule wameripoti tukio hilo kwa maafisa wa polisi eneo hilo.

Comments

comments