Magavana Wahimiza Kaunti za Kaskazini Mashariki Kuchangia Sekta ya Elimu.

Magavana Wahimiza Kaunti za Kaskazini Mashariki Kuchangia Sekta ya Elimu.

by -
0 305

Baraza la magavana linataka serikali za kaunti ziruhusiwe kudhibiti elimu katika maeneo yaliyoathiriwa na ukosefu wa usalama kaskazini mashariki mwa nchi.

Mwenyekiti wa baraza hilo Isaac Ruto amesema ipo haja kwa serikali za kaunti kuchangia kwa kuajiri walimu ambao ni wakaazi wa maeneo hayo ili shughuli za masomo ambazo zimesambaratika, ziendelee.

Ruto amekosoa tume ya kuwaajiri walimu nchini, TSC, kwa kuwashurutisha walimu kurejea maeneo hayo licha ya wao kuhusi hakuna usalama.

Walimu wanaofanya kazi kaskazini mashariki hasa Mandera walidinda kurudi kazini baada wenzao kushambuliwa na kuuawa na wanamgambo wa Al Shabaab mwaka jana.

Amesisitza kwamba mchakato kuhusu kura ya maoni ya kuimarisha pesa mashinani, ungali upo, licha ya serikali kuongeza mgao wa fedha kwa kaunti hadi shilingi bilioni 58.

Comments

comments