Jamii Ya Wamakonde Kusajiliwa Rasmi

Jamii Ya Wamakonde Kusajiliwa Rasmi

by -
0 1198

Serikali imezindua rasmi zoezi la kusajili jamii ya Wamakonde waishio hapa Pwani ya Kenya, wengi wakiwa na asili kutoka nchi ya Msumbiji.

Zoezi hilo limeratibiwa kufanyika kwa muda wa wiki moja kuanzia alhamisi hii februari 12, katika kaunti kadhaa hapa Pwani,ambazo ni Kwale,Kilifi na Taita Taveta.

Katika wilaya ya Msambweni kaunti ya Kwale ambako jamii hiyo inalalamikia kunyimwa vitambulisho, usajili umeanza katika eneo la Kinondo,karibu na kijiji cha Makongeni ambako jamii hiyo inaishi.

Jamii hiyo ya Wamakonde imekuwa ikilalama kuwa imenyimwa vitambulisho vya uraia wa Kenya,wakitajwa kuwa ni wageni waliotoka nchi ya Msumbiji.

Rais Uhuru Kenyatta alipotembelea kaunti ya Kwale,alionyesha nia ya kusikia kilio cha Wamakonde ndio sababu usajili huu unafanyika.

Historia inaonyesha kuwa Wamakonde wa kwanza kutoka Msumbiji,walizuru Kenya mwaka 1936 na kusajiliwa na wakoloni kufanya kazi katika mashamba makubwa ya makonge huko Taveta,Vipingo na Msambweni.

Comments

comments