Dhamana Yafutiliwa Mbali

Dhamana Yafutiliwa Mbali

by -
0 335

Mahakama kuu hapa Mombasa imefutilia mbali dhamana waliopewa washukiwa Wanne wa ulanguzi wa dawa za kulevya.

Katika uamuzi wake jaji Anyada Emukule ameagiza upande wa mashtaka na washukiwa kwenda katika mahakaama ya rufaa, ili kupata mwelekeo kuhusu kesi hiyo.

Jumanne mchana kiongozi wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko kupitia wakili wa serikali Alexander Muteti, alipinga uamuzi wa mahakama kuwaachia washukiwa hao kwa dhamana ya shilling million 30.

Dhamana ya kwanza waliyokuwa wamepewa na mahakama ndogo ilikuwa ya shilingi milioni tano kila mmoja, lakini ofisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma ilipokata rufaa mahakama kuu dhamana hiyo ikaongezwa hadi shilingi milioni 30.

Wana wawili wa marehemu Ibrahim Akasha pamoja na washukiwa wengine wawili wanakabiliwa na kesi ya ulanguzi wa dawa za kulevya, humu nchini na Marekani.

Kuna kesi nyingine ambapo wanahitajika kusafirishwa nchini Marekani kujibu tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya, na kesi hiyo itasikizwa Februari tahere 16.

Comments

comments