Mwindaji Haramu Auawa Taita Taveta.

Mwindaji Haramu Auawa Taita Taveta.

by -
0 621

Maafisa wa shirika la huduma kwa wanyama pori nchini, KWS kaunti ya Taita Taveta, wamemuua mshukiwa mmoja wa uwindaji haramu katika mbuga ya wanyamapori eneo la Choke.

Afisa msimamizi wa mbuga ya Tsavo, Dickson Too amesema mshukiwa aliuawa kwa kupigwa risasi huku wenzake wawili wakitoroka.

Washukiwa wanadaiwa kumfuma mishale ya sumu ndovu mmoja siku chache zilizopita na tayari walikuwa waeng’oa pembe zake.

Duru zimearifu kwamba washukiwa walipatikana na bunduki aina ya AK47 na risasi kadhaa.

Comments

comments