Vijana Wahamasishwa Kuhusu Muungano wa Afrika.

Vijana Wahamasishwa Kuhusu Muungano wa Afrika.

by -
0 411

Mashirika 10 ya kijamii kutoka hapa barani Afrika yameungana kufanya kampeini ya kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa maswala yanayoangaziwa katika muungano wa mataifa ya Afrika AU.

Kampeini hiyo imepewa jina “Be the voice” na itazinduliwa rasmi kesho katika chuo kikuu cha Pwani mjini Kilifi ikilenga kuzuru vyuo vikuu mbali mbali hapa Afrika.

Msanii maarufu Nazizi aliteuwa kama balozi wa kampeini hiyo ambayo inalenga hasa vijana kote barani.

Mwangi Maina, afisa mkuu wa shirika la Fahamu ambalo litaongoza kampeni hiyo jijini Nairobi, amesema wanatarajia kuelimisha vijana kuhusu maswala 14 yanayoathiri vijana hapa nchini na Afrika, ikiwemo ukosefu wa ajira na utumizi wa mihadarati.

Comments

comments