Kesi ya Uchochezi Dhidi ya Mishi Mboko Yahairishwa.

Kesi ya Uchochezi Dhidi ya Mishi Mboko Yahairishwa.

by -
0 1369

Mahakama ya Mombasa imeahirisha kesi ya uchochezi inayomkabili mwakilishi wa wanawake katika bunge la kaunti ya Mombasa Mishi Mboko.

Wakili wake Jared Magolo amearifu mahakama kwamba Mboko alikuwa nje ya nchi na hivyo kuomba mahakama ihairishe kesi yake.

Wakili wa serikali Alexander Muteti hakupinga ombi hilo na badala yake amethibitisha kwamba upande wa mshtakiwa ulikuwa umewasilisha barua rasmi ikiarifu kuhusu kutokuwepo kwa mshtakiwa.

Hakimu Richard Odenyo amekubali ombi hilo na kuagiza kesi hiyo itajwe juma lijalo.

Mboko anadaiwa kutoa matamshi ya uchochezi kwa umma katika hafla ya kuadhimisha siku kuu ya Madaraka mwaka jana.

Alikana mashtaka na akaachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki nne na wadhamini wawili au shilingi laki mbili pesa taslimu.

Comments

comments