Bunge lapendekeza NYS watumiwe kusimamia kitengo cha trafiki nchini.

Bunge lapendekeza NYS watumiwe kusimamia kitengo cha trafiki nchini.

by -
0 425

Kamati ya bunge kuhusu usalama sasa inapendekeza kitengo cha huduma ya vijana kwa taifa NYS kichukue nafasi ya polisi wa trafiki kudumisha sheria na usalama katika barabara za nchi hii.

Kamati hiyo inasema pendekezo hilo linalenga kupunguza ufisadi kwa kuwaondoa polisi ambao wameshtumiwa kujihusisha na uovu huo.

Mwenyekiti wa kamati Asman Kamama amesema polisi wa trafiki wanaohusishwa na ufisadi wanapaswa kuondolewa kutoka idara hiyo na kupewa kazi zingine.

Akizungumza hapa Mombasa, Kamama amesema polisi hao hutumia vizuizi vya barabani kuwapora madereva.

Comments

comments