Viongozi wa Jumuiya ya Kaunti za Pwani kukutana wikendi hii.

Viongozi wa Jumuiya ya Kaunti za Pwani kukutana wikendi hii.

by -
0 937

Muungano wa Jumuiya Ya Kaunti Za Pwani unatarajiwa kukutana na viongozi wote wa kaunti sita za pwani mjini Voi wikendi hii, kuzungumzia mafanikio na malengo ya muungano huo.

Mwenyekiti Salim Mvurya amesema wanatayarisha mswaada utakaowasilishwa na kujadiliwa katika mabunge ya kaunti zote, na pia kuwasilishwa kwa uma kabla ya uzinduzi wa muungano huo mwezi Machi.

Mkutano huo utakuwa ni wapili baada ya wa kwanza kuandaliwa mjini Lamu Desemba mwaka jana.

Comments

comments