Nkaissery Ahairisha Ziara Yake Lamu.

Nkaissery Ahairisha Ziara Yake Lamu.

by -
0 413

Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery amehairisha tena ziara yake kaunti ya Lamu mara kwa muda usiojulikana.

Nkaissery alitarajiwa kuzuru Lamu Jumatatu ijayo lakini akahairisha ziara hiyo ili kutoa nafasi kwa viongozi wa Lamu kutatua migogoro iliyokuwepo kati yao na afisi ya kaimu kamishna wa kaunti ya Lamu, Fredrick Ndambuki.

Viongozi wa kaunti ya Lamu wakiongozwa na gavana Issa Timamy wamekuwa wakimshtuu kaimu kamishna kwa kile wanachodai kama kuto waheshimu.

Wiki jana waliapa kutojihusisha na Nkaissery iwapo angefika eneo hilo, wakidai hawakujulishwa kuhusu ziara yake eneo hilo.

Waziri alikuwa amepangiwa kukutana na kaimu kamishna wa kaunti hiyo Ephantus Kiura, machifu na viongozi wa mpango wa Nyumba Kumi, kuhusu hali ya usalama eneo hilo.

Comments

comments