WANAFUNZI WA NAIROBI AVIATION WAKAMATWA.

WANAFUNZI WA NAIROBI AVIATION WAKAMATWA.

by -
0 379

Takriban wanafunzi 18 wa taasisi ya Nairobi Aviation wamekamatwa na polisi jijini Nairobi, walipokuwa wakiandamana kupinga makala iliyoonyeshwa na runinga moja nchini ikidai taasisi hiyo inatoa vyeti bandia vya masomo.

Wanafunzi hao waliandamana hadi jumba la Nation Center wakidai waonyeshwe vyeti ambavyo makala hiyo ilionyesha kuwa gushi.

Iliwalazimu polisi watumie gesi za kutoa machozi kutawanya wanafunzi hao waliorusha mawe kwenye jumba hilo na kuvunja vioo na milango.

Wanafunzi hao wanadai makala hiyo ilinuiaya kuwaathiri kitaaluma, na kuwakosesha ajira katika siku za usoni.

Comments

comments