Wenye mashamba taita watisha kwenda mahakamani kusitisha ujensi za barabara

Wenye mashamba taita watisha kwenda mahakamani kusitisha ujensi za barabara

by -
0 257

Mamia ya wamiliki wa mashamba katika maeneo ya Ndilidau, Majengo na Salaita  kaunti ya Taita Taveta wametishia kwenda mahakamani kusimamisha mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwatate-Taveta.

Wenyeji hao wanadai kutofidiwa licha ya ardhi zao kutwaliwa kwa minajili ya kujenga barabara hiyo, na wanalaumu serikali kwa kupuuza vilio vyao.

Ujenzi wa barabara hiyo ya kilomita 80 unadhaminiwa na Africa development bank  kwa gharama ya shilingi bilioni 10.

Wenyeji wanadai serikali imekataa kuwafidia kwa kisingizio cha kuwepo kwa mzozo kuhusu mmiliki halisi wa ardhi hizo.

Comments

comments