Wanafunzi waonywa kuepuka mihadarati

Wanafunzi waonywa kuepuka mihadarati

by -
0 429

Wanafunzi wa shule za upili katika kaunti ya Kilifi wameonywa kujiepusha na utumizi wa mihadarati hasa wakiwa shuleni.

Afisa mkuu wa polisi kaunti ya Kilfi Justine Nyaga amesema anatamaushwa na ongezeko la visa vya wanafunzi wa shule kupatikana wakitumia mihadarati shuleni na nyumbani.

Nyaga anawataka wazazi kuwajibikia zaidi tabia za watoto wao, na akaonya kwamba wazazi huenda wakachuliwa pia hatua katika visa vinavyohusu watoto wao.

Amesema mikakati inaendelea kuwajumuisha viongozi katika hamasisho dhidi ya utumizi wa mihadarati hasa baina ya vijana hasa wanafunzi.

Comments

comments