Waathiriwa wa uvamizi lamu wakata tamaa kuhusu fidia

Waathiriwa wa uvamizi lamu wakata tamaa kuhusu fidia

by -
0 467

Wenye majengo yaliyoteketezwa na magaidi Mpeketoni, kaunti ya Lamu mwezi Juni na Julai mwaka uliopita sasa wanasema wamekata tamaa kuhusu majengo yao kukarabatiwa, miezi saba baada ya serikali kutoa ahadi hiyo.

Wafanyabiashara hao pia wanadai kampuni za bima zimekataa kuwalipa fidia na zinadai kwamba hawakuwa wamechukua bima dhidi ya ugaidi.

Mwezi Juni mwaka jana, waziri wa ugatuzi na mipango Anne Waiguru alizuru eneo hilo na kuahidi kwamba serikali kupitia kwa wizara yake ingekarabati majengo hayo.

Lakini wakizungumza na Baraka FM, waathiriwa wanasema serikali imekuwa kimya kuhusu ahadi hiyo, na kwamba wameshindwa kuinua tena biashara zao.

Comments

comments