Washukiwa Al-Shabaab waachiliwa kwa dhamana

Washukiwa Al-Shabaab waachiliwa kwa dhamana

by -
0 370

Mahakama ya Mombasa imewaachilia kwa dhamana ya shilingi laki 5 kila mmoja, vijana watano waliokamatwa katika msikiti Musa kwa madai ya kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al Shaabab.

Hakimu Justus Kituku amesema makosa yanayowakabili washukiwa yanawaruhusu kupewa dhamana kisheria.

Amesema upande wa mashtaka haukutoa sababu za kurudhisha mahakama kuwanyuma washukiwa dhamana.

Hakimu Kituku hata hivyo amewaagiza vijana hao kuripoti kwa afisa mchunguzi wa kesi hiyo Charles Mwai, mara mbili kila mwezi.

Vijana hao wanadaiwa kupatikana na vilipuzi katika msikiti Musa eneo la Majengo, Novemba mwaka jana, na pia wanahusishwa na kundi la Alshabaab.

Comments

comments