Wanaoishi katika ardhi ya uwanja wa ndege kuhama.

Wanaoishi katika ardhi ya uwanja wa ndege kuhama.

by -
0 336

Takriban familia 24 ambazo zingali zinaishi katika eneo lililotengewa uwanja wa ndege wa Manda katika kaunti ya Lamu zimetakiwa kuhama mara moja.

Meneja wa uwanja huo Mohamed Lippi, amesema familia hizo zimekuwa zikitatiza shughuli za ki-usalama katika uwanja wa Manda licha ya kufidiwa na serikali.

Kauli hiyo imeungwa mkono na idara ya polisi eneo hilo ambayo inasema juhudi za kudumisha usalama uwanjani humo zimetatizwa na kuwepo kwa familia hizo.

Comments

comments