Mkataba wa kujenga mradi wa maji

Mkataba wa kujenga mradi wa maji

by -
0 483

Serikali ya kaunti ya Taita Taveta imetia sahihi mkataba na serikali ya Uhispania, kuhusu ujensi wa mradi wa maji utakaogharimu takriban shilingi bilioni 10.

Gavana wa kaunti hiyo John Mruttu amesema wawekezaji hao wamelenga kukarabati vyanzo vya maji vya Mzima springs, Ziwa Challa na Njoro ili kuongeza kiwango cha maji katika maeneo hayo.

Mruttu amesema mradi huo utasaidia katika unyunyizaji mashamba maji, na kumaliza mzozo uliopo kati ya wanyama pori na binadamu.

Maeneo yalioathirika zaidi na uhaba wa maji ni Kasighau, Maktau, Kishushe, Mwatate na Mbololo.

Comments

comments